Kwanza uongozi wa Yanga umewapa heshima kubwa ya kutambulisha nyota wapya waliosajiliwa siku ya mwisho kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa
Mwanatanga na familia yako jongea hapo uwanja wa Mkwakwani uwe sehemu ya matukio yanayokwenda kujiri leo
Nje ya uwanja unaweza kujipatia jezi halisi za Yanga kutoka kwa GSM, lakini pia unaweza kujiandikisha kuwa Mwanachama wa Yanga kupitia Kilinet
Baadae ingia uwanjani kusubiri utambulisho rasmi ya 'suprise' ya usajili iliyoandaliwa leo
Jioni utapata burudani ya kandanda safi kutoka kwa mabingwa wa kihistoria, Yanga watakapo wakabili Coastal Union katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Leo Wanatanga wapenda soka wanakutana Mkwakwani...!
ADVERTISE HERE