Jioni ya leo kikosi cha Yanga kinashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kucheza na Mbuni Fc katika mchezo wa kirafiki
Ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa Jumapili mkoani Moshi
Mapema kabla ya mchezo huo hapo uwanjani kutakuwa na zoezi la mashabiki wa Yanga kujiandikisha kwa ajili ya kupata Uanachama wa klabu
Mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni na utarushwa mbashara na Azam Sport 1 HD
ADVERTISE HERE