Fiston Mayele ndiye kinara wa kupachika mabao ligi kuu ya NBC msimu huu akiweka kambani mabao sita
Mayele aliwapiku washambuliaji wengine baada ya kufunga bao katika mchezo dhidi ya Coastal Union uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mkoani Tanga
Mayele anastahili kuwa hapo kileleni kwa mpaka sasa amedhihirisha ndiye mshambuliaji hatari zaidi
Kama hatapata majeraha ya aina yoyote anayo kila sababu ya kuibuka mfungaji bora msimu
Kwani kwa wastani Mayele anafunga katika kila mchezo anaokuwa uwanjani

ADVERTISE HERE