Mlinzi wa kshoto wa Yanga David Bryson jana alishindwa kumaliza mchezo dhidi ya Mbuni Fc baada ya kufanyiwa madhambi mapema kwenye kipindi cha kwanza
Lilikuwa tukio la rafu mbaya ya kukanyagwa mgongoni ambalo lilipelekea mchezaji wa Mbuni Fc aliyefanya madhambi hayo kutolewa nje kwa kadi nyekundu
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wa klabu, Bryson anaendelea vizuri lakini leo atapelekwa hospitalini kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kubaini madhara aliyopata
Bumbuli amesema winga Chico Ushindi nae alipata majeraha, atafanyiwa uchunguzi pia
"Bryson anaendelea vizuri baada ya matibabu aliyopewa na madaktari wetu lakini leo watampeleka hospitalini akafanyiwe uchunguzi wa kina kubaini madhara ambayo anaweza kuwa ameyapata. Chico Ushindi nae alipata majeraha kidogo," alisema Bumbuli
Yanga imeweka kambi mkoani Arusha kujiandaa na mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambao huenda ukahamishiwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumapili, Januari 23, Moshi