Jana mashabiki wa Yanga walimshuhudia kiungo Mapinduzi Balama 'Kipenseli' akirejea uwanjani baada ya kukosa kumuona kwa takribani miezi 18
Balama alicheza dakika 45 za kipindi cha pili mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni Fc uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
Kilichowafurahisha wengi ni kiwango bora alichoonyesha Balama katika mchezo huo
Balama amepitia nyakati ngumu katika kipindi chote alichokuwa akitibiwa majeraha ya kifundo cha mguu
Ilifika kipindi hata mwenyewe alikata tamaa ya kurejea uwanjani kutokana na aina ya majeraha aliyokuwa amepata ambapo alilazimka kufanyiwa upasuaji mara mbili
Bila shaka Kocha Nasreddine Nabi ataendelea kumpatia nafasi hata katika michezo ya ligi kuu na michuano mingine ili kumuimarisha zaidi
Jambo muhimu ni kumuona amerejea uwanjani tena akiwa katika ubora uleule