Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ratiba ya raundi ya nne ya mechi za kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambapo Yanga itakipiga na Mbao Fc inayoshiriki ligi daraja la pili
Wananchi watakuwa nyumbani katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi ya Januari 29, 2022 saa moja usiku
Ushindi utaihakikishia Yanga kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo ambayo bingwa atajihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

ADVERTISE HERE