Tumefuata alama tatu Arusha - Hafidh

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2022
Tumefuata alama tatu Arusha - Hafidh

Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema timu inaendelea vyema na mazoezi mkoani Arusha kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania ambao utapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumapili

Hafidh amesema wameweka malengo ya kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi

Akizungumza baada ya mazoezi ya jioni ya leo yaliyofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Hafidh alisema wachezaji wote wako katika afya timamu kukiwa hakuna mchezaji majeruhi

"Tunashukuru tunaendelea vizuri na mazoezi, wachezaji wote wako sawa, wote wameshiriki mazoezi ya leo, naweza kusema hatuna mchezaji majeruhi"

"Tumekuja hapa Arusha tukiwa na lengo moja, kuhakikisha tunashinda mchezo huo. Hatujali takwimu za michezo iliyopita, muhimu ni kuwa Jumapili Januari 23, utakuwa mchezo mpya ambao sisi tunatizama kushinda zaidi," alisema Hafidh

Polisi Tanzania tayari wametangaza viingilio vya mchezo huo ambapo VVIP -20,000/=,  VIP A&B - 10,000/= na MZUNGUKO- 5,000/=

Tiketi zinapatikana kupitia N- CARD katika Vituo Vifuatavyo; Sheikh Amri Abeid Stadium, Ofisi za TTCL Arusha na MOSHI- Ofisi za TTCL

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’