Baada ya kurejea kutoka Arusha hapo jana, wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja wakitarajiwa kurejea kambini kesho Jumatano kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo wa raundi ya nne utapigwa Jumamosi, Januari 29 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, kuanzia saa moja usiku
Msimu huu Wananchi wamedhamiria kushinda mataji yote ya ndani, wakianza na Ngao ya Jamii ambayo tayari iko kabatini pale Jangwani
Bado mataji ya ligi na kombe la FA ambayo yote yanashikiliwa na watani zao Simba
ADVERTISE HERE