Msimu huu Wananchi wacha watambe kwani wana watu! Ndio wana watu aisee! Baada ya machungu ya misimu minne iliyopita, msimu huu ni wao
Ubora wa kikosi cha Yanga unachangiwa na uwepo wa wachezaji wengi mahiri na wenye uzoefu mkubwa
Yannick Bangala na Khalid Aucho ni miongoni mwa wachezaji hao
Injini ya kikosi cha Nasreddine Nabi katika eneo la kiungo, ni Aucho na Bangala
Katika mchezo wowote ambao utawaona wawili hao wakianza pamoja, basi tarajia burudani ya aina yake itakayoambatana na ushindi
Ni mchezo mmoja tu dhidi ya Simba kwenye ligi ambao Aucho na Bangala walikuwepo lakini Yanga haikushinda
Mafundi wawili ambao timu pinzani hazitamani kuwaona uwanjani zinapocheza na Yanga
ADVERTISE HERE