Jumamosi hii Yanga inashuka uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao Fc katika mchezo wa raundi ya nne kombe la FA
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kushinda ili kutinga hatua ya 16 bora
Yanga imelazimika kuupeleka mchezo huo Mwanza kutokana na uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa na matumizi mengine
Mbao Fc imekuwa na historia ya kipekee inapocheza na Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba
Hivyo pamoja na kuwa sasa wako daraja la pili, Yanga haipaswi kudharau mchezo huu
Katika kipindi chote ambacho Mbao Fc walishiriki ligi kuu Yanga ilishinda mchezo mmoja tu dhidi yao hapo CCM Kirumba
Hivyo kocha Nasreddine Nabi na benchi lake la ufundi wanapaswa kuchukua tahadhari zote kuhakikisha Wananchi wanaondoka na furaha jijini Mwanza
ADVERTISE HERE