Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema lengo kuu ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo yao bila ya kujali matokeo ya wapinzani wao
Nabi amewaonya wachezaji wake kuwa hawapaswi kujadili matokeo ya wapinzani wao kwani sio jambo muhimu kwao
"Nimewaambia wachezaji sitaki kusikia hata wanazungumza ishu za Simba kwani matokeo yao hayatuhusu na nimewataka wazingitie na kufikiria zaidi mechi zetu zinazotukabili"
"Nimewaambia kabisa nikimkuta mchezaji yeyote anafanya hivyo au mtu yeyote katika benchi langu la ufundi akijadili Simba au timu nyingine juu ya matokeo yao nitawapa adhabu zilizopo kwenye miongozo yao ya kazi"
"Yanga tuna mechi zetu ambazo sasa zitazidi kuwa ngumu, nimewaambia kuanzia sasa kila mchezo utakaokuwa mbele yetu utakuwa ni sawa na fainali ngumu ambazo ni lazima tuzishinde," alisema Nabi
Yanga imejifunza kutokana na makosa yaliyotokea misimu ya nyuma hasa msimu uliopita ambao waliongoza kwa muda mrefu lakini hawakuweza kutwaa ubingwa
Msimu huu wamejipanga kuhakikisha wanashinda kila mchezo ili kuweza kutwaa ubingwa sasa wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 10