Fiston Mayele ameipeleka Yanga hatua ya 16 bora michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Mbao Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Krosi murua ya Farid Mussa aliyekuwa katika kiwango bora, ilitua kichwani mwa Fiston katika dakika ya 54

Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi huku Mbao Fc wakijilinda zaidi na kutumia mashambulizi ya kushitukiza
Baada ya kuwakosa katika kipindi cha kwanza, Yanga ilirejea na kasi zaidi kwenye kipindi cha pili kwani licha ya bao alilofunga Mayele, kulikuwa na nafasi nyingi ambazo zingeweza kuipa Yanga ushindi mnono zaidi
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa na mabadiliko makubwa, nyota wengi wakikosekana kutokana na sababu mbalimbali
Mvua iiyonyesha kabla ya mchezo na hata wakati wa mchezo, haikuwazuia Wananchi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia mchezo huo