Baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya 16 bora michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kuichapa Mbao Fc bao 1-0, Yanga itakumbana na Biashara United katika mchezo wa raundi hiyo
Biashara United wameichapa Mbeya Kwanza mabao 2-1 hivyo kunasa katika mtego wa kukutana na vinara hao wa ligi kuu ya NBC
Mchezo baina ya timu hizo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kati ya Februari 15-22
Yanga na Biashara United tayari zimekutana uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi na Yanga kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1
ADVERTISE HERE