Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga mwishoni mwa wiki hii Jumamosi, Februari 05 watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo wa raundi ya 14
Yanga ilirejea kutoka jijini Mwanza jana ambako walifanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kombe la FA kwa kuichapa Mbao Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Wananchi wameanza maandalizi kuwakabili Mbeya City ambao msimu huu umekuwa mzuri sana kwao
Mbeya City wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu msimu huu
Walifanikiwa kuwalaza na viatu Simba kwa kuwachapa bao 1-0 mkoani Mbeya na kuwalazimisha Azam Fc sare ya mabao 2-2 pale Azam Complex
Hivyo ni moja ya mechi ngumu ambayo Yanga inahitaji kushinda iili kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi