Huyu Mayele ni hatari sana - kipa Mbao Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jan 2022
Huyu Mayele ni hatari sana - kipa Mbao Fc

Mlinda lango wa Mbao FC, Wandwi Jackson amesema Fiston Mayele ni mchezaji hatari ambaye ataendelea kuzinyanyasa timu pinzani kama safu zao za ulinzi hazitakuwa makini nae

Mayele alifunga bao pekee la Yanga katika mchezo wa kombe la FA akimtungua mlinda lango huyo na kuipeleka Yanga hatua ya 16 bora.

Wandwi amesema kwa dakika zote 90 alizokuwa golini mtu ambaye alikuwa hatari zaidi ni Mayele kutokana na mikimbio yake na kujua kukaa kwenye maeneo ambayo ni hatari kama mabeki hawakuwa makini.

"Huyu jamaa yupo vizuri chini, yupo vizuri juu, wakati wenzake wana mpira, yeye anajua wapi aende kukaa ili iwe rahisi kwake kucheza. Halikimbii goli, muda wote wenzake wakitaka kupiga krosi yupo golini, ndiyo maana nilikuwa nawapigia kelele sana mabeki wangu na kuwakumbusha wamchunge sana kwa sababu wachezaji wote wa Yanga ndiyo wanamtegemea yeye na kumpigia yeye tu krosi, na jinsi anavyopambana kuipata mipira.

"Niliwaambia mkizembea wakati wowote anaweza kutudhuru na kweli, mpira huo huo wa krosi ndiyo uliotudhuru kwa kosa moja tu," alisema Wandwi

Mayele amefunga mabao sita kwenye ligi kuu akiwa anashika nafasi ya pili nyuma ya Reliants Lusajo wa Namungo Fc mwenye mabao saba

Katika mechi zote akiwa na Yanga msimu huu, Mayele amehusika katika mabao 18

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’