Yanga imedhamiria kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), uongozi umesisitiza kuwa watakwenda hatua kwa hatua
Mwezi huu wa Februari 2022, Yanga itacheza michezo minne ambapo michezo mitatu ni ya ligi kuu na mchezo mmoja ni kombe la FA
Februari 05, Jumamosi Wananchi watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Mbeya City katika mchezo muhimu ambao alama tatu kwa Yanga zitakuwa na maana kubwa katika mbio za ubingwa
Mbeya City iliweza kupata ushindi dhidi ya Simba, mpinzani namba moja wa Yanga katika mbio za ubingwa
Lakini pia wakapata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Azam Fc, timu nyingine ambayo bado haijakata tamaa na mbio za ubingwa licha ya kuachwa alama 14 na Yanga
Baadae Yanga itahamishia nguvu zake kombe la FA kusaka nafasi ya kutinga robo fainali katika mchezo dhidi ya Biashara United ambao utapigwa kati ya Februari 13-17 2022
Mtibwa Sugar wataialika Yanga kule Manungu, Turiani Februari 23 katika mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kushinda
Mchezo wa mwisho kwa mwezi Februari ni dhidi ya Kagera Sugar, Februari 27 ambao utakuwa mchezo wa kwanza wa duru ya pili utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
