Kiungo wa Yanga Feisal Salum amesema yuko imara kiafya baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa na yuko tayari kuwatumikia Wananchi
Feisal amesema yuko tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa kama kocha Nasreddine Nabi atampa nafasi
"Mimi nimepona kabisa na nimerejea mazoezini na wenzangu. Nawaahidi mashabiki wa Yanga nitaendelea kuipigania timu kama mwanzo"
"Kuelekea mchezo wa Jumamosi, mimi niko tayari, kama mwalimu atanipatia nafasi, nitacheza," alisema Feisal
Gazeti moja la kila siku juzi liliandika taarifa kuwa Feisal amepata majeraha na atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne
Feisal amekanusha taarifa hiyo na kusisitiza yuko timamu kiafya, amekuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Mbeya City