Mmesikia watu wameshangilia sare huko?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2022
Mmesikia watu wameshangilia sare huko?

Mashabiki wa Yanga hawakufurahishwa kabisa na matokeo ya suluhu ya bila kufungana ambayo timu iliyapata dhidi ya Mbeya City hapo jana

Lakini kwa upande wa wapinzani wao Mbeya City, kwao ilikuwa shamrashamra ya aina yake

Mtu asiyefahamu anaweza kudhani Mbeya City wametwaa ubingwa kwa aina ya shamra shamra waliloshusha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo

Hii ni ishara ya heshima na ukubwa wa Yanga. Kwa mara ya pili msimu huu tunaona timu inashangilia kupata alama moja dhidi ya Yanga!

Lakini pia kwa upande mwingine, ni ujumbe kwa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa Yanga kuwa vita ya ubingwa msimu huu ni kubwa

Kuanzia sasa wafahamu kuwa Yanga inaposhuka uwanjani kucheza mechi yoyote ya ligi, hawachezi na timu moja

Kila timu watakayokutana nayo itaandaliwa vyema kuhakikisha inawatibulia mipango yao. Mbeya City waliwekwa kambini jijini Dar es salaam kwa wiki mbili kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga

Mechi za Yanga sasa zitakuwa ngumu sana kwa sababu watakuwa wakikabiliana na upinzani mara dufu

Wachezaji waongeze ukatili mbele ya lango la wapinzani, watumie kila nafasi wanayopata kufunga

Zimebaki mechi 16 kukamilisha msimu huu, hizo zote ni mechi za fainali kwa Yanga

Kwa mashabiki wakati wa kushangilia ubingwa bado, huu ni wakati wa kuhamasisha na kusapoti timu kuhakikisha alama tatu zinapatikana katika kila mchezo

Hesabu za ubingwa zifanyike mwezi May 2022 pale msimu utakapomalizika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’