Mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Mayele amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi Januari 2022
Katika mwezi huo Yanga ilicheza mechi tatu, mbili za ligi kuu na moja ya kombe la FA ikifanikiwa kushinda michezo yote huku Mayele akifunga mabao mawili
Tuzo ya kocha bora wa mwezi Januari 2022 imechukuliwa na Francis Baraza, mkufunzi wa Kagera Sugar
Mayele amekuwa na msimu mzuri katika kikosi cha Yanga mpaka sasa akiwa amefunga mabao sita katika ligi kuu ya NBC

ADVERTISE HERE