Kampuni ya GSM imetangaza rasmi kujitoa kudhamini ligi kuu ya NBC baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushindwa kutekeleza makubaliano ya kimkataba
Taarifa iliyotolewa na GSM mbele ya waandishi wa habari leo, imebainisha kuwa kukiukwa kwa baadhi ya vipengele vya mkataba kumepelekea GSM kuchukua uamuzi huo mgumu
Hata hivyo GSM itaendelea kuzamini klabu za ligi ambazo wana makubaliano nazo
Katika hatua nyingine, Ghalib Said Mohammed (GSM) nae amejiuzulu nafasi ya Mwenyekiti na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya timu ya Taifa kuanzia leo Februari 7, 2022Β
ADVERTISE HERE