Msitupendelee, tendeni haki, msituonee - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Feb 2022
Msitupendelee, tendeni haki, msituonee - Manara

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema Yanga haihitaji upendeleo wa aina yoyote kutoka kwa Bodi ya Ligi lakini wangependa kuona haki inatendeka katika usimamizi wa ligi ili kila timu ipate haki yake

Manara ameyasema hayo leo katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam

Manara amesema kumekuwa na mijadala kila mara kuhusu mwenendo wa waamuzi wanaochezesha mechi za ligi kuu msimu huu

Manara amesema kuwa Yanga na viongozi hawatoi malalamiko kwa Waamuzi ila wanafanya hivyo kuwakumbusha tu kwa kuwa Klabu yao ina mashabiki na wanaona haki haitendeki na wao kazi yao ni kusema kwa kuwa ndio Kazi ambayo wameichagua

"Nilifanya press, niliwasihi Wanayanga kote nchini tusiende kulalamika, nilisema waziwazi mimi binafsi nina imani na TFF na Bodi ya Ligi, huwa sipendi kuwa sehemu ya watu wanaokosoa mamlaka zinazosimamia mpira ndio maana niliwaambia twende tukacheze tukiamini ubora wa kikosi chetu bila kulalamika"

"Kuna matukio yasiyopungua 9 mpaka 10 yanayohusisha mechi za Simba ambazo watu wamelalamika kama watu wanavyolalamika kwenye mechi zingine hatuna shida na hilo lakini hiyo humanity iwe kwa timu zote"

"Refa wa mechi ya Yanga na Namungo aliadhibiwa hawa wa matukio mengine hawajachukuliwa hatua, wa mechi na Polisi alichukuliwa hatua Kwa sababu hakutoa red card kwa Djuma," alihoji Manara

"Kuna mechi Simba waliomba kutocheza kwa sababu wachezaji wao wanaumwa, siku iliyofuata sisi tunacheza Sumbawanga"

"Hakuna mechi ngumu tuliyocheza kama ile ya Prisons wachezaji wameingia wanaumwa lakini tuliambiwa hamjafuata utaratibu jinsi ya kuomba"

"Wamecheza kina Mwamnyeto na mapanadol Sita Sita, mchezaji akitoka Half Time anakula Panadol anakula Diclopar," aliongeza Manara

Manara amesisitiza kuwa Yanga haichezi ligi kwa lengo ya kutopoteza mchezo, malengo waliyojiwekea ni kutwaa ubingwa.

Manara amehoji kwa nini kuwa ikitokea timu pinzani inawafunga au kutoka sare kwenye mchezo dhidi ya Simba inaonekana kuwa timu hiyo imetumwa na imeahidiwa kupatiwa pesa kufanya hivyo?

Amefafanua kuwa, kinachotokea ni kwamba Simba huwa inataka kushinda kila mchezo lakini ukubwa wanaojipa kunawafanya kuwa kwenye hali hiyo ila timu zote ni sawa utofauti ni rangi za jezi na majina tu

"Sasa wenzetu ikitokea kwao wao, utasikia kumeahidiwa fedha hii, nyie nani? Kwa nini mshinde kila mechi?, mna nini?, Nyie ukubwa mnaojipa mmeupata wapi ?, Upi ?, Ukubwa na una-hustle dakika ya 90 na inapigwa mpaka dakika ya 97 pale, Ukubwa upi mnauzungumza?"

"Sisi Hatuchezi ligi hii kuwa unbeaten tunacheza kuwa champion, Sisi ni klabu ya mpira lazima tutafungwa, Ni wenzetu tu ambao wanaamini wakifungwa wamehujumiwa, Sisi tunajua hii ni klabu ya mpira lazima kuna siku utapigwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’