Kwanza ni jambo la kupongeza kwa viongozi wa Yanga na wadau walioanzisha jithada za michakato mbalimbali ya kuisaidia Yanga wakati ilipokuwa katika kipindi kigumu
Michakato hiyo iliwaleta GSM ambao baadae wakajitokea kusimamia mchakato mzima wa mabadiliko kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla
Sasa Yanga iko kwenye hatua ya kuandikisha Wanachama katika mfumo wa kidigitali ambapo zoezi hilo linaendelea nchini nzima
Kulingana na taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, hadi kufikia wiki iliyopita, takribani Wananchi 9600 walikuwa wameandikishwa kuwa Wananchama wa Yanga ikiwa ni mwezi mmoja tangu zoezi la uandikishaji lilipoanza
Kiasi cha fedha zilizokusanywa ni takribani Sh270, 504, 258/- yaani zaidi ya Milioni 270
Kama Yanga itafanikiwa kuandikisha angalau Wananchama laki moja tu basi itakusanya takribani Bil 2.9
Kwa hakika mchakato huu wa Yanga utakuwa mfano kwa wengine kwani mpaka sasa tayari umeanza kuonyesha mafanikio mapema tu ukiwa bado haujakamilishwa kwa asilimia 100
Kwani baada ya zoezi la kuandikisha Wanachama ndipo wawekezaji wataalikwa baada ya kufanyika tathmini ya thamani ya klabu