Klabu zalia GSM kusitisha udhamini Ligi Kuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Feb 2022
Klabu zalia GSM kusitisha udhamini Ligi Kuu

Baadhi ya vilabu vikubwa vya Ligi kuu ya NBC Tanzania vimetaka mazungumzo ya kumrejesha GSM yafanyike kufuatia Mdhamini huyo mwenza kujiondoa

GSM ilijiondoa kama mdhamini mwenza kwa kile kilochodaiwa kuwa TFF ilishindwa kuheshimu baadhi ya masharti ya mkataba yaliyokibaliwa

Kufuatia hilo wadau wa soka wamekuwa na maoni tofauti huku wengi wakitaka mazungumzo ya haraka kati ya GSM na TFF kufanyika na kurekebisha kasoro zilizopo ili kuirejesha GSM katika nafasi yake.

Afisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alibainisha kuwa kuondoka kwa GSM ni pigo kubwa kwa vilabu

"Waungane kutafuta suluhu kwani ligi inahitaji wadhamini wengi na sio kuwapoteza " alisema Bwire huku akikiri hawakuwa wameanza kupokea fedha kutoka GSM tangu mkataba huo usainiwe

Kwa upande mwingine Katibu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe alisema ameshangazwa na kitendo cha GSM kujiondoa katika nafasi hiyo akiamini pande husika zitakaa kutafuta muafaka

"Ni kweli hatujapokea kiasi chochote kutoka kwao lakini hilo sio suala kubwa kwasababu tulijua muda wowote tungeweza kupata sehemu yetu kulingana na matakwa ya mkataba"

Aidha, Kimbe amesema changamoto nyingine inayovikabiki vilabu ni suala la nembo ya GSM kuwepo kwenye jezi za timu hizo, jambo ambalo litalazimisha kuingia gharama ya kutengeneza upya jezi zao kwa kuondoa nembo ya GSM.

Mwenyekiti wa Biashara United, Selemani Mataso kwa sehemu yake amesema wanasubiri kusikia TFF itakuja na tamko gani

"Kwa upande wetu hatuna mengi ya kusema kuhusu kujiengua kwa GSM bali tunataka kuona TFF itatoa maamuzi gani."

Mapema Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB), Stephen Mguto alipoulizwa kuhusu majibu aliirushia mpira TFF akisema wao ndio wapo katika nafasi nzuri ya kutolea maelekezo wakati TFF ikisisitiza bado inaliangalia suala hilo kabla ya kutoa tamko

Credit : Maulid Kitenge

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’