Msemaji wa Yanga Haji Manara amewataka Wanachama na Mashabiki kuendelea kuisema na kuipigania timu ili kuhakikisha wanatimiza malengo waliyojiwekea msimu huu
Manara amesema ni jukumu la kila Mwanayanga kuwa sehemu ya kutimiza dhamira hiyo, ambayo ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC na kombe la Shirikisho la Azam
Jumanne ya wiki ijayo Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Biashara United katika mchezo wa hatua ya 16 bora michuano ya kombe la Shirikisho la Azam
Manara amesema wanafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha Biashara United lakini wanahitaji kushinda waweze kutinga robo fainali
ADVERTISE HERE