Leo ni miaka 87 tangu ilipoundwa klabu ya Yanga, Februari 11, 1935. Hapo awali Yanga ilianzishwa kwa lengo la kuwa sehemu ya kupigania uhuru wa Tanganyika kwa kupitia michezo kutokana na nyakati hizo ilikuwa hairuhusiwi watu kukusanyika na kujadili maswala mbali mbali ya ukombozi
Asili ya kuitwa timu ya Wananchi imetokana na historia hiyo ya kuanzishwa kwake kwani wakati ule wa harakati za kudai Uhuru hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliitumia Yanga kama sehemu ya kukutana na kujadili harakati za ukombozi
Yanga imekuwa na mafanikio makubwa kuliko klabu yoyote ndani ya ardhi ya Tanzania, ukizungumzia timu yenye makombe mengi, utaitaja Yanga. Kwa historia yake pia hakuna timu yenye mashabiki wengi hapa Tanzania kuizidi Yanga
Baada ya kupitia katika changamoto nyingi, hatimaye mwaka huu Yanga imeandika historia nyingine kwa kuwa klabu ya kwanza kufanya Mabadiliko ya kweli ya mfumo wake wa uendeshaji
Wakati huu zoezi la kuandikisha Wanachama katika mfumo mpya wa kidigitali linaendelea na baadae litafuata zoezi la kuandikisha mashabiki wa klabu
Yanga itafanya upya tathmini ya thamani yake ya sasa kabla ya kuwaalika wawekezaji ambao watanunua hisa asilimia 49 huku hisa asilimia 51 zikiendelea kubaki mikononi mwa Wananchama
Imekuwa miaka 87 yenye milima na mabonde lakini sasa ni wazi inakoelekea Yanga ni kuzuri zaidi kuliko huko ilikotoka
HAPPY BIRTHDAY YANGA...!