Tukio la kumnyaga kwa bahati mbaya kwenye mbavu Richardson Ng'ondya wa Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu, limepelekea mlinzi Dickson Job kufungiwa michezo mitatu kulingana na adhabu zilizotolewa na kamati ya usimamizi na uendeshaji wa ligi kuu ya NBC
Job pia ametozwa faini ya Tsh 500,000/- kutokana na kosa hiyo
Anaungaza na mlinzi Djuma Shabani ambaye atamaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu kwa kukosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United, Jumanne ijayo
Job atakosa michezo dhidi ya Biashara United, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar
Katika hatua nyingine, Yanga imetozwa faini ya Tsh 1,000,000/- baada ya mashabiki kuwarushia chupa za maji waamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City
Aidha waamuzi wa mchezo huo Hussein Athumani (kati) na Godfrey Msakila (2), wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguuko mitatu baada ya kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Nao Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli na Msemaji Haji Manara wametozwa faini ya Tsh 500,000/- kila mmoja kwa kosa la kuwashutumu waamuizi wa ligi kuu ya NBC