Tunasikitika kutangaza kifo cha Sentahafu wetu wa zamani Ally Mtoni Sonso kilichotokea kwenye Hospitali kuu ya Taifa ya Muhimbili.
Msiba wa Ally Sonso upo nyumbani kwao Magomeni Kondoa, Dar es Salaam. Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo February 12, 2022 saa 10 jioni kwenye makaburi ya Ndugumbi, Magomeni.
Sonso anakumbukwa kwa mengi klabuni ikiwemo ujasiri wake ndani ya Uwanja, nidhamu pamoja na kujitolea kuipigania Jezi ya Yanga
"Tunamuombea kwa Mungu aipokee roho ya mpendwa wetu Ally na pia tunatoa pole kwa wafiwa wote, hususan familia yake. Inna lillah Wainna Ilaihi Raajiuun"

ADVERTISE HERE