Baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliopita dhidi ya Tiger Queens, Yanga Princess leo itashuka uwanja wa Mabatini kuikabili Mlandizi Queens katika mchezo ambao kinadada hao kutoka mitaa ya Twiga na Jangwani wanazihitaji alama zote tatu
Msimu huu Yanga Princess wameuanza kwa kusuasua, wanahitaji kupata matokeo katika michezo yao mitano ya viporo ili kurejesha imani ya mashabiki wao kwao
Katika michezo mitano waliyocheza Yanga Princess, wameshinda mechi mbili, wametoka sare mechi mbili na kupoteza mchezo mmoja

ADVERTISE HERE