Uongozi wa Azam Media umethibitisha wafanyakazi wake waliokuwa wakisafiri kwenda mkoani Mbeya kwa ajili ya kazi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya NBC wamepata ajali baada ya gari lao kusukumwa na lori lililokuwa likirudi nyuma kwa dharula katika Mlima Kitonga, Iringa
Taarifa iliyotolewa na Azam Media imebainisha kuwa ajali hiyo imetokea mchana wa leo Jumapili, Februari 13, 2022
"Kwa msaada mkubwa wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kikosi cha Polisi Mkoa wa Iringa na Mganga mkuu wa Mkoa, majeruhi wamechukuliwa na matabibu wa Mkoa wa Iringa kwa matibabu"
"Uongozi wa Azam Media Limited unawashukuru wote waliotoa msaada wa hali na mali na kuwaomba Watanzania wote kuwaombea majeruhi nafuu ya mapema," ilibainisha sehemu ya taarifa hiyo
Tunawapa pole Azam Media kwa ajali iliyowakumba wafanyakazi wake, tunawaombea kwa Mwenye ez Mungu ili waweze kupona haraka na waweze kuendelea na majukumu yao