Mlinzi wa kulia wa Yanga Mkongomani, Djuma Shaban ataanza kuonekana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar Februari 23, akitarajiwa kumaliza adhabu ya kufungiwa michezo mitatu kwa kukosa mchezo wa kombe la FA dhidi ya Biashara United kesho
Djuma alirejea mapema kikosini baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa na amekuwa akifanya program maalum ya mazoezi ili kuhakikisha anarudi kikosini akiwa imara zaidi
Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kurejea kwa Djuma kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ni jambo jema katika kikosi chake kwani ni mchezaji mwenye mchango mkubwa
Hata hivyo Nabi amesema amelazimika kuzungumza na wachezaji wake akiwataka kuzuia hasira hata pale wanapochokozwa uwanjaniΒ
"Wachezaji wangu karibia wote wanachezewa vibaya kwa kupaniwa na wachezaji wa timu pinzani, hivyo nisingependa kuwaona wakiwa na jazba mara baada ya kuchezewa vibaya kwa kurudishia"
"Nilizungumza na Djuma naamini jambo kama lile halitajitokeza tena kwani matukio ya aina ile yanaigharimu timu kwa kuwakosa wachezaji wake muhimu," alisema Nabi
Wakati Djuma akimaliza adhabu hapo kesho, mlinzi Dickson Job yeye ataanza adhabu ya kukosa michezo mitatu