Yanga imetinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa raundi ya tano uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabao mawili yaliyopatika kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Yannick Bangala na Fiston Mayele yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu katika mchezo ambao Yanga ilitawala
Yanga ilikuwa bora sana kwenye kipindi cha kwanza kama isingekuwa makosa ya 'kibinadamu' ya waamuzi, pengine ingekwenda mapumziko ikiwa na idadi kubwa ya mabao
Bao pekee la Biashara United lilifungwa na Opare kwenye dakika ya 38 baada ya kiungo Khalid Aucho kuchelewa kuondoa hatari langoni
Yanga iliendelea kulisakama lango la Biashara United katika kipindi cha pili lakini dakika 90 zikashuhudia mchezo huo ukimalizika kwa ushindi huo wa Yanga



