Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema Mabadiliko yaliyofanywa na klabu ya Yanga yatakuwa mfano kwa klabu nyingine na yanakwenda kuifanya Yanga kuwa taasisi imara kiuchumi
Akizungumza jana katika uzinduzi wa kadi za Yanga za ki-elektroniki uliowahusisha Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ni Wanachama wa Yanga, Senzo alisema mchakato huo umeongeza thamani ya klabu
Amesema kuanza sasa wanatarajia hata wale wadhamini watakaopenda kufanya kazi na Yanga watapaswa wajipange kwani sasa wanafahamu thamani yao
Akizungumza katika hafla hiyo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, Dominic Albinius ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi alisema wameanza kutoa kadi Bungeni kwa kuwa ndiko hata wazo la mchakato wa mabadiliko lilipoanzia.
Mwenyekiti tawi la Yanga Bungeni, Seif Gulamali alisema wabunge ambao ni wanachama wa klabu hiyo waliojiandikisha wapo 120, lakini kati ya hao baadhi tayari waliomba kujiandikisha kwenye matawi yao