Yanga imethibitisha kuwa nyota wake watatu Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu na Denis Nkane, wako mbioni kurejea kikosini baada ya afya zao kuimarika
Wachezaji hao ni miongoni mwa takribani wachezaji 10 ambao walikosekana katika mchezo uliopita kutokana na sababu za majeruhi na nyinginezo
Nkane bado hajacheza mchezo wowote wa ligi tangu aliposajiliwa na Yanga wakati wa dirisha dogo
Alipata majeraha kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwezi uliopita
Ninja na Kibwana wao walifanyiwa upasuaji mdogo mwezi uliopita nchini Tunisia, wamefanya program maalum za mazoezi kwa wiki kadhaa
Wachezaji wengine ambao bado ni majeruhi ni pamoja na Chrispine Ngushi, Yassin Mustafa, David Bryson na Yassin Mustafa
ADVERTISE HERE