Kazi nzuri iliyofanywa Nasreddine Nabi katika kikosi cha Yanga imemuhakikishia mkataba mpya ambao atausaini wakati wowote
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinius amesema tayari wamefikia makubaliano na Nabi, atasaini mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi
"Unajua zipo timu zinatamani kuwa na kocha kama huyu hata humu ndani zipo, sasa sisi kama Kamati tumewaambia uongozi wa juu uchukue hatua haraka kwani hata kocha amekubali"
"Ni vigumu sana kupata makocha kama hawa na sisi kama Yanga hatutaki kufanya makosa, tuna mpango wa muda mrefu nae ndio maana hata katika sajili alizofanya karibuni amesajili wachezaji wa mpango wa muda mrefu," alisema Albinus
Mkataba wa mwaka mmoja aliosaini mwaka jana utaisha mwishoni mwa mwezi April, lakini yuko tayari kusaini mkataba mpya kuendelea kubaki Jangwani
Tangu alipojiunga na Yanga, Nabi amepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi dhidi ya Azam Fc msimu uliopita
Msimu huu Yanga bado haijapoteza mchezo ikiwa na malengo ya kwenda 'unbeaten' msimu mzima