Vinara wa ligi kuu ya NBC Yanga watacheza na Geita Gold mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Mchezo huo namba 89 utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kama Wananchi watashinda mchezo huo huenda wakakutana na watani zao Simba kwenye mchezo wa nusu fainali
Simba itacheza na Pamba Fc hatua ya robo fainali, mchezo namba 90 ambao pia utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo wa hatua ya nusu fainali kati ya mshindi wa mchezo namba 89 dhidi ya mshindi wa mchezo namba 90 utapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Mchezo wa robo fainali namba 91 ni kati ya Azam Fc dhidi ya Polisi Tanzania wakati mchezo namba 92 ni kati ya Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo wa nusu fainali kati ya mshindi wa mchezo namba 91 dhidi ya mshindi wa mchezo namba 92 utapigwa uwanja wa CCM Kirumba
Mechi za robo fainali zitapigwa kati ya April 08-13 2022