Klabu ya Yanga kupitia wadhamini wake GSM, wametangaza punguzo kubwa la mauzo ya jezi ambapo bei ya rejareja sasa ni Tsh 30,000/- badala ya 35,000/- ya awali
Msemaji wa Yanga Haji Manara alitangaza punguzo hilo leo katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika GSM Salamander Tower jijini Dar es salaam
Pia kuna punguzo la mauzo ya jezi za jumla ambapo sasa mzigo unapatikana kwa Tsh 22,000/-
Sambamba na taarifa hiyo, Yanga imezindua wimbo rasmi wa hamasa, YANGA TAM ulioimbwa na Mario
Mario msanii wa bongofleva anayetamba na kibao chake cha Bia Tam, nae ametangaza kuwa yeye ni Mwananchi...!

ADVERTISE HERE