Mshambuliaji kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga Fiston Mayele, amewaahidi mashabiki wa timu hiyo kuwa watapambana kufa au kupona katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar na kuhakikisha wanashinda.
Itakuwa mara ya kwanza kwa nyota wa Yanga kucheza katika uwanja wa Manungu ambao ulitumika kwa mara ya mwisho mwaka 1999 katika mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga
Mayele amesema licha ya kufahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini watapambana kama timu kuhakikisha wanaibuka na ushindi kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wenyewe.
"Tunafahamu ukubwa wa mchezo huu, ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi, hivyo tunatakiwa kuumaliza kwa ushindi, naona utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini lakini hatuhofii hilo"
"Sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano na tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunaondoka na ushindi, kila mchezo kwetu unahitaji ushindi, na hiyo ni kutokana na kuhitaji kutimiza malengo yetu msimu huu, "alisema Mayele
Mayele amefunga mabao sita kwenye ligi sasa akiwa nyuma kwa tofauti ya mabao manne dhidi ya Reliants Lusajo anayeongoza mbio za kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao 10