Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro
Akizungumza na Wanahabari katika Mkutano Maalum wa mechi, Kaze amesema ni mchezo ambao wamejipanga wakiwa na dhamira ya kushinda
"Tunaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya mchezo lakini jambo muhimu ni kuwa na kiwango bora katika muda wote wa mchezo. Wachezaji wetu wanafahamu umuhimu wa mchezo huu, ushindi hauwezi kuja wenyewe tutapaswa kupambana ili kuupata," alisema Kaze
ADVERTISE HERE