CAF yataja Waamuzi Watakaochezesha Mechi ya Yanga na Saint Louis FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2018
CAF yataja Waamuzi Watakaochezesha Mechi ya Yanga na Saint Louis FC
Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi watakaochezesha mchezo wa kwanza na wa pili wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Yanga ya Tanzania dhidi ya Saint Louis FC ya Seychelles.

Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 10, 2018 uwanja wa Taifa na utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia na Kamishna wa mchezo akitokea nchini Namibia.

Mwamuzi wa kati atakuwa Belay Tadesse Asserese akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Tigle Gizaw Belachew na mwamuzi msaidizi namba mbili Kinfe Yilma Kinfe wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Amanuel Heleselass Worku na Kamishna Frans Vatileni Mbidi.

Mechi ya pili itakayochezwa Seychelles kati ya Februari 20 na 21,2018 itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar na kamishna atatoka Mauritius.

Mwamuzi wa kati atakuwa Andofetra Avombitana Rakotojaona akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Lionel Hasinjarasoa Andrianantenaina na mwamuzi msaidizi namba mbili Pierre Jean Eric Andrivoavonjy na mwamuzi wa akiba Hamada el Moussa Nampiandraza,kamishna wa mchezo huo Ahmad Nazeer Hossen Bowud.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’