Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo aliamua kubadili pacha yake kwenye eneo la kiungo kwa kuanza na Khalid Aucho na Salum Abubakar 'Sure boy'
Nabi hakukosea kuanza na Sureboy leo na pengine anaweza kubadili mawazo yake anapochagua mtu wa kumtumia sambamba na Aucho pale Bangala anaporudishwa kwenye eneo la ulinzi
Sure boy anakuhakikishia jambo moja, pasi zake ni za uhakika na mara nyingi ni za kuelekea mbele
Nabi hupendelea kumtumia Zawadi Mauya zaidi katika eneo hilo lakini katika michezo ya hivi karibuni, umakini wa Mauya hasa katika kupiga pasi haukuwa mzuri
Bao la pili lililofungwa na Fiston Mayele katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar leo, aliyeanzisha shambulizi hilo ni Sure Boy ambapo pasi yake mahiri kwa Saido ilifungua safu ya ulinzi ya Mtibwa Sugar
Hii Yanga ina watu! katika kila eneo kuna wachezaji wawili au zaidi ambao wanakupa uhakika wa huduma bora uwanjani