Baada ya ushindi wa kibabe uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar es salaam jana tayari kuanza duru ya pili ligi kuu ya NBC kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumapili, Februari 27 2022 kuanzia saa moja usiku
Yanga imefunga hesabu za duru ya kwanza kibabe na sasa Jumapili imepania kuanza kukusanya alama katika ngwe ya lala salama
Ni nafasi kwa Yanga kuweza kutwaa ubingwa kama itatumia vyema mechi nyingi watazocheza uwanja wa Benjamin Mkapa katika duru ya pili
Yanga imebakisha michezo minne tu ya kucheza nje ya jiji la Dar es salaam katika duru ya pili
ADVERTISE HERE