GSM, TFF wakaa upya mezani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Feb 2022
GSM, TFF wakaa upya mezani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanya mazungumzo na kampuni ya GSM ili warejeshe udhamini wao kwenye ligi kuu ya NBC, imefahamika

Februari 07, GSM ilitangaza kujiondoa rasmi kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania bara kutokana na kutotimizwa kwa makubaliano ya Mkataba baina yao na Shirikisho la soka nchini (TFF)

Mmoja wa viongozi wa TFF amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti, ambapo amesema kuwa tayari wameanza mazungumzo ya kuona ni namna gani GSM atarejea kuendelea kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu

"Kinachofanyika sasa ni kuona ni namna gani changamoto zilizojitokeza zinawekwa sawa na mazungumzo yanakwenda vizuri na kuna matumaini kwa kiasi fulani wa kupata muafaka wa jambo hili ili GSM arudi Ligi Kuu," alisema

Katika taarifa iliyotolewa na GSM wakati wakitangaza kujitoa, ilionyesha klabu ya Simba ndio iliyokiuka makubaliano hayo ya mkataba kama kutoweka mabango na kuvaa nembo ya GSM

Pia katika mikutano yao na wanahabari Simba walikuwa hawaweki nembo ya GSM kama sehemu ya wadhamini wa ligi

Mkataba wa udhamini wa GSM na TFF ulikuwa na thamani ya Tsh Bili 2.1 

Licha ya GSM kujitoa bado klabu zimeendelea kuvaa nembo ya GSM pamoja na kuweka mabango jambo linaloashiria kuwa mgogoro huo huenda utamalizwa na GSM kuendelea kuwa mdhamini mwenza wa ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’