Jana njioni viongozi wa Yanga walimtembelea mtoto Ali Kimara maarufu Ali Yanga ambaye ni shabiki kindakindaki wa Yanga
Juzi kituo cha televisheni cha chaneli 10 kiliripoti kuhusu mtoto huyo anayegua kwa takribani miaka nane sasa akiwa kitandani
Lakini maradhi hayo hayajazuia mapenzi yake kwa Yanga ambapo familia yake wanasema ni shabiki kwelikweli wa Yanga ambaye hakosi kuwatizama Yanga wakicheza kupitia simu yake
Msafara huo wa viongozi uliambatana na mshambuliaji Fiston Mayele kwa niaba ya wachezaji wengine
Kwa hakika ni tukio lenye thamani kubwa kwa mtoto Ali
ADVERTISE HERE