Mlinzi Djuma Shabani na kiungo Khalid Aucho wanaweza kuukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba kesho Jumapili kutokana na changamoto ya kuugua
Hata hivyo mlinzi Kibwana Shomari ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na timu, huenda akarejea kikosini katika mchezo huo
Yanga ilifanya mazoezi yake jana katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo nyota wote waliosafiri na timu walishiriki
Dickson Job amemaliza adhabu yake kama ilivyo kwa Feisal Salum ambao wote wako tayari kwa mchezo huo
Kama Aucho atakosekana ni wazi Yannick Bangala atachukua nafasi yake katika eneo la kiungo huku Job akirejea katika safu ya ulinzi
Kibwana anaweza kuanza nafasi ya Djuma kama Mcongomani huyo atakosekana katika mchezo huo
ADVERTISE HERE