Yanga kamili kuivaa Azam FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2018
Yanga kamili kuivaa Azam FC
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwenye dimba la Uhuru kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC.

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumamosi katika dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam ukitarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.



Baada ya mchezo huo, Yanga inakabiliwa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Lipuli FC Feb 03 kabla ya kuivaa St Louis Februari 10 kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika.

Yanga iliyoweka kambi maalumu kwa ajili ya mchezo huo wa keshokutwa imekuwa ikijifua kwa nguvu chini ya kocha wake George Lwandamina.

Lwandamina amesema atatumia michezo hiyo miwili kukipima kikosi chake kiko tayari kiasi gani kuelekea michuano ya ligi ya mabingwa.



Msimu huu uongozi wa Yanga umeweka malengo ya kuhakikisha timu inatinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya Mabingwa.

Kama Yanga itatinga hatua ya makundi ina uhakika wa kujizolea zaidi Mil 500 achilia mbali mapato itakayopata kutokana na michezo itakayocheza katika hatua ya makundi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’