Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema wamejiwekea malengo ya kushinda ubingwa msimu huu hivyo wameiandaa timu kuhakikisha wanatimiza lengo hilo
Senzo ameeleza kushangazwa na propaganda zilizoibuliwa kabla ya mchezo dhidi ya Geita Gold kudai Yanga imenunua mchezo huo
Amesema maneno kama hayo yanazungumzwa pale unapofanya vizuri kwa sababu wapo wengi tu ambao hawafurahishwi kuiona Yanga ikifanya vizuri
"We umeangalia mchezo umeuonaje? Tumefunga goli la mapema na wachezaji wetu wamejitoa kwa zaidi ya asilimia 100. Ulikuwa mchezo mgumu sana lakini tumejilinda vizuri na kuweza kupata ushindi"
"Sisi hatusikilizi hayo wanayosema kwani malengo tuliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu tunaendelea kuyatekeleza vyema na tutaendelea kujipanga ili tuafanye vizuri katika kila mchezo unaokuja mbele yetu," alisema Senzo
Naye Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema propaganda hiyo ilianzishwa na wapinzani wao Simba wakiamini kwa kusema Geita Gold wameuza mechi basi watawafanya wapambane kupata matokeo ili kuthibitisha kuwa hawakuwa wameuza mchezo huo
Pengine hilo lilichangia Geita Gold kucheza kwa nguvu kubwa lakini uimara wa Yanga ulidhihiri baada ya dakika 90 kwa kuibuka na ushindi