Baada ya kurejea jijini Dar es salaam wakitokea Mwanza, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ametoa mapumziko ya siku mbili kwa wachezaji
Jumatano Yanga inatarajiwa kuanza maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya KMC ambao utapigwa March 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kurejea kutoka Mwanza ambako alikiongoza kikosi cha Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold, Nabi alisema wachezaji wanahitaji mapumziko hayo ili kurejesha utimamu wa mwili baada ya kucheza mechi ngumu
Aidha wapo wachezaji walipata majeraha katika mchezo huo wao watapewa mapumziko ya siku zaidi ili kuhakikisha wanakuwa sawa
Kuelekea mchezo dhidi ya KMC, Nabi amesema anatarajia baadhi ya wachezaji ambao walikosekana katika mchezo uliopita, watakuwa wamerejea kikosini
Jana katika mchezo dhidi ya Geita Gold, Yanga iliwakosa wachezaji 10 kutokana na sababu za majeruhi na maradhi