Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kwa upande wao wamekwisha kamilisha upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi (57).
Mbali na Malinzi wengine wanakabiliwa na kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine (46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga (27).
Wakili wa Takukuru, Leonard Swai jana alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa wao kama Takukuru wamekamilisha upelelezi kwenye kesi hiyo na kwamba hadi Jumatatu jalada la kesi hiyo litakuwa limerejeshwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Swai alidai kuwa awali jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kulirejesha Takukuru kwa maelekezo ambapo wameyafanyia kazi.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 8, 2018.
Washtakiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29,2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha Dola za Marekani 375,418.
Katika kesi hiyo, Malinzi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka 28 ya uhujumu uchumi ikiwamo kughushi na utakatishaji wa fedha dola za Marekani 375,418.
Katika kesi hiyo Malinzi wanakabiliwa na mashtaka 28 huku wenzake wakikabiliwa na makosa yasiyozidi manne.
Wakati kesi hiyo ikitajwa washtakiwa wote walikuwapo mahakamani na wanatetewa na mawakili Nehemia Nkoko, Dokinician Rwegoshora na Abraham Senguji.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE