Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi cha Yang leo kinaanza mawindo ya mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumatano, March 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni mchezo wa raundi ya 18 ikiwa ni hatua ya lala salama kuhitimisha ligi kuu ya NBC msimu wa 2021/22
Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi, inahitaji kushinda mchezo huo ili kulinda dhamira ya kutwaa ubingwa msimu huu
Wananchi wameanza na rekodi ya ushindi kwa asilimia 100% katika michezo ya duru ya pili wakizifunga Kagera Sugar (3-0) na Geita Gold (1-0)
Yanga ilishinda mabao 2-0 katika mchezo wa duru ya kwanza dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa Majimaji, Songea
ADVERTISE HERE