Mshambuliaji wa Yanga Chrispine Ngushi ameanza mazoezi na wenzake baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa
Tangu aliposajiliwa na Yanga dirisha dogo mwezi Januari 2022, Ngushi hajawa na mwenendo mzuri wa kiwango alichokuwa nacho Mbeya Kwanza kutokana na changamoto hiyo ya majeraha
Ngushi amethibitisha kuanza mazoezi akiwa tayari kuwatumikia Wananchi baada ya kuona majeraha
Msimu huu Ngushi amepachika mabao matatu ligi kuu ya NBC yote akiyafunga wakati akiitumikia Mbeya Kwanza kwenye duru la kwanza
Ni mmoja wa wachezaji waliomvutia kocha Nasreddine Nabi hivyo kupendekezwa asajiliwe
ADVERTISE HERE